Videoz nyingi zinasambaa mtandaoni na Instablog9ja zimeonyesha baadhi ya 'miujiza' yaliyofanywa na Ugochukwu Emmanuel Ekwem wiki chache zilizopita ili kuweka kando tamaa za kibinafsi na kutoa kipaumbele kwa mambo ya taifa.
Katika kanda hiyo, waumini wanaonyeshwa wakianguka chini kila alipokuwa akinyoosha mikono yake upande wao akiwa kwenye madhabau.
Video ilionyesha wakati anakimbia kwenye upande wa kwaya, akanyoosha mkono wake upande wao na kisha wote walianguka.
Ugochukwu aliingia katika sehemu nyingine ya kanisa na kuwagusa na upako wake.
Yote yalikuwa kama kipindi cha kawaida cha televisheni cha wachungaji wakionyesha jinsi walivyo na vipawa vya kiroho.
Pasta huyo alikamatwa akiwa safari kuja Kenya kwa krusedi ya wiki tatu jijini Nairobi akipatikana na vifurushi 54 za dawa za kulevya mwilini mwake.