Mahakama ya kijeshi nchini Sudan imemuhukumu kifungo cha miaka tisa gerezani mkuu wa majeshi wa zamani wa taifa hilo, Hashem Abdel-Muttalib Babakr na maafisa wengine watano miaka mitano kila mmoja kwa kukutwa na hatia ya kufanya jaribio la mapinduzi lililoshindwa la 2019. Kesi hiyo ilianza Julai 2019, miezi mitatu baada ya jeshi kumpindua kiongozi wa muda mrefu wa Sudan, Rais Omar al-Bashir, wakati wa maandamano ya wananchi dhidi ya utawala wake uliopewa nguvu na wenye itikadi kali. Watawala wa kijeshi wa sasa nchini humo wanasema jaribio la mapinduzi lililoshindwa lilihujumu mgawanyo wa madaraka baada ya makubaliano kati ya majenerali na vuguvugu la kuunga mkono demokrasia.