Ukraine inaishtumu Marekani kwa kusaidia Urusi, baada ya kutoipa taarifa kuhusu makombora yanayolenga nchi yake.
Rais Volodymyr Zelensky, amesema pia hatua ya Bilionea wa Marekani Elon Musk kusitisha huduma za mtandao wa Starlink, unaisaidia Urusi kwenye vita hivyo.
Zelensky ambaye amekuwa ziarani nchini Uingereza, amemtaka Musk kurejesha huduma za Starlink, ambazo zimekuwa muhimu kufuatilia makombora kutoka Urusi.
Hata hivyo, Musk amesema Marekani iko nyuma ya kuzuia huduma za starlink ambayo imeathiri matumizi ya silaha za Ukraine.
Hivi karibuni afisa wa juu wa Kyiv alithibitisha kuwa, Marekani ilitishia kuacha kutoa taarifa za kiiteljensia kuhusu makombora yanayoruhswa na Urusi, madai ambayo haya hivyo Trump amekanusha.