Wizara ya Hazina ya Marekani imeiwekea vikwazo Wizara ya Ulinzi ya Rwanda na Benki ya Zigama kwa kuunga mkono waasi wa M23 mashariki mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Katika yake kwa Vyombo vya habari Waziri wa Hazina wa Marekani Scott Bessent amesema Rwanda lazima ikomeshe usaidizi wake kwa M23 na kuondoa wanajeshi wake RDF kutoka mashariki mwa DRC
Idara yake ilitangaza vikwazo vipya vinavyolenga Wizara ya Ulinzi ya Rwanda na Jumuiya ya Mikopo na Akiba ya Zigama, taasisi ya kifedha ya Rwanda. Kwa hivyo, mali na maslahi yao yote nchini Marekani yamezuiliwa.
Washington inadai kuwa Wizara ya Ulinzi ya Rwanda imekuwa ikifadhili na kusaidia operesheni za kijeshi za kundi la waasi la M23 na muungano wa AFC mashariki mwa DRC, ambayo hivi karibuni yalijumuishwa katika muungano unaofahamika kama FRN ambayo Washington inasema haiitambui.
Marekani inaishutumu Jumuiya ya Mikopo na Akiba ya Zigama, taasisi ya kifedha ya Rwanda kwa kurahisisha ununuzi wa silaha na kufanikisha miamala ya mamilioni ya dola iliyofaidisha makundi hayo ya waasi.
Hatua hizi zinasababisha kuzuiliwa kwa mali zote za taasisi hizo zilizo chini ya mamlaka ya Marekani pamoja na kupiga marufuku miamala yote ya kifedha inayohusisha taasisi hizo na raia au mashirika ya Marekani.