Watu wasiopungua 60 wafa katika ajali ya treni Congo

Watu wasiopungua 60 wamethibitishwa kufariki baada ya treni ya mizigo kutoka kwenye njia yake katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Ajali hiyo ilitokea siku ya Ijumaa wakati treni hiyo, ambayo ilikuwa inasafiri kati ya vijiji vya Kitenda na Buyofwe katika mkoa wa Lualaba, ilipoacha njia wakati inapanda kilima na kuanguka kwenye korongo. Kiongozi wa eneo hilo Clementine Lutanda, ameliambia shirika la habari la Ujerumani, dpa hapo jana, kwamba mabehewa saba kati ya 10 yalinguka kwenye korongo, na kuongeza kuwa bado kulikuwa na miili iliyokwamba kwenye vifusi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii