Mfugaji NarudashwaTitika mwenye umri wa miaka 45 mkazi wa kijiji cha Alaitore kilichopo ndani ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha amefariki dunia baada ya kushambuliwa na mnyama aina ya tembo sehemu mbalimbali za mwili wake.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi MKoa wa Arusha ACP Justine Masejo amesema kuwa tukio limetokea Machi 9, 2022 majira ya saa saba mchana.
ACP Masejo amesema Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa marehemu alikutwa na mkasa huo wakati akitafuta kuni akiwa na wenzake ndani ya hifadhi ndipo alipo shambuliwa na tembo huyo, mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi baada ya uchunguzi wa daktari.
Katika tukio jingine Machi 9, 2022 majira ya saa nne asubuhi
katika kitongoji cha Karafia kijiji cha Kisimiri Wilaya ya Arumeru Mkoa
wa Arusha askari wakiwa katika operesheni walifanikiwa kuharibu shamba
lenye ukubwa wa ekari tano (05) likiwa na miche idhaniwayo kuwa madawa
ya kulevya aina ya bhangi.
ACP Masejo amesema kuwa mtuhumiwa wa shamba hilo aliyefahamika
kwa jina moja la Babu alitumia mbinu ya kuchanganya miche hiyo ya bhangi
pamoja na mazao aina ya mahindi, ambapo juhudi za Jeshi la Polisi
mkoani Arusha linaendelea kumtafuta mmiliki wa shamba hilo ili hatua za
kisheria zichukuliwe dhidi yake.