Rigathi akata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama

Aliyekuwa naibu rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, amekata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama kuu iliyounga mkono kuondolewa kwake madarakani akisema uamuzi wa jopo la majaji watatu ulikiuka haki zake za kikatiba .

Katika rufaa yake, Gachagua anasema mahakama kuu ilikosea kuukubali uamuzi wa bunge la seneti kumuondoa madarakani, licha ya mahakama hiyo kubaini kuwa haki zake za kikatiba zilikiukwa.

Kuhusu ushirikishwaji wa raia, Gachagua anadai kuwa wananchi hawakushrikishwa kikamilifu, akidai muda uliowekwa na bunge uliathiri ushiriki wa umma na haki yake ya kusikilizwa.

Aidha kiongozi huyo anapinga uteuzi wa Kithure Kindiki kuwa naibu rais , pamoja na fidia ya shillingi Millioni 50 iliyoamriwa na mahakama kuu akitaja kuwa fidia hiyo haitoshi kutetea haki zake za kikatiba.

Gachagua sasa anaiomba mahakama ya rufaa itangaze uamuzi wa seneti  wa Oktoba 17 2024 kuwa batili.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii