Watu 50 wamepoteza maisha nchini Nigeria, baada ya boti kuzama katika jimbo la Sokoto, Kaskazini Magharibi mwa Nigeria, siku ya Alhamisi.
Abdulkadir Yusuf, Meneja wa mamlaka ya safarini za majini, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo karibu na eneo la Gorau.
Boti hiyo ilikuwa inawasafirisha wakulima na wafanyazi wao, waliokuwa wanafanya kazi kwenye mashamba ya mpunga.
Abiria zaidi ya 70 walikuwa kwenye boti hiyo, wakiwemo watoto wenye umri kati ya miaka 10 hadi 15. Watu wengine 16 waliokolewa baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Ajali za boti nchini Nigeria hutokea mara kwa mara, kwa sababu ya ubovu wa boti na kupakia mizigo na abiria kupita kiasi.