Bunge la Ufaransa limeidhinisha muswada wa sheria utakaopiga marufuku watoto wenye umri wa chini ya miaka 15 kutumia mitandao ya kijamii.
Hatua hiyo inafainya Ufaransa kuwa taifa la kwanza la Ulaya kutunga sheria itakayowazuia watoto kwenye mitandao kama TikTok.
Rais Emmanuel Macron alipigia debe kupitishwa sheria hiyo akiitaja kuwa alama ya mageuzi aliyoahidi katika muhula wake wa pili wa urais na amesema utekelezaji wake utaanza Septemba mwaka huu.
Ameusifu uamuzi wa bunge la nchi hiyo wa kupitisha muswada huo akisema "Ufaransa inaongoza njia barani Ulaya linapohusika suala la kuwalinda watoto na vijana balehe."
Idadi inayoongezeka ya nchi duniani zinachukua hatua za kuzuia matumizi ya mitandao ya kijamii hasa kutokana tahadhari zinazotolewa juu ya madhara yake wa watoto.