Rais Joseph Aoun wa Lebanon amekutana na Rais Donald Trump wa Marekani mjini Washington wakati wa ziara yake ya kutafuta uungwaji mkono katika kuishiniza Israel kuondoa vikosi vyake ndani ya Lebanon.
Auon ambaye ni kiongozi wa kwanza wa Lebanon kualikwa kufanya ziara nchini Marekani tangu mwaka 2009, ametumia mkutano huo na Trump kusisitiza haja ya Israel kuondoa jeshi lake kwenye ardhi ya taifa lake akisema uhuru wa Lebanon ni lazima uheshimiwe.
Trump kwa upande wake ameahidi kuisaidia Lebanon akisema taifa hilo limetendewa vibaya kwa miongo miongo kutokana na kushambuliwa kila wakati.
Rais Aoun anashinikiza kupata uungwaji mkono katika utekelezaji wa makubaliano kati ya Lebanon, Israel na Marekani yaliyofikiwa wiki za karibuni yanayotaka Israel kuondoa wanajeshi wake huku Lebanon ikiwa na jukumu la kulipokonya silaha kundi la Hezbollah.