Uingereza yafuta mazozi ya kila mwaka ya wanajeshi wake Kenya

Uingereza imefuta mazoezi ya kila mwaka ya wanajeshi wake nchini Kenya, baada ya kutopata leseni kutoka kwa utawala wa Nairobi.

Wizara ya Ulinzi wa Uingereza imethibitisha hatua hiyo siku ya Alhamisi, ambapo imesema inasikitika kuwa mazoezi ya kila mwaka ya wanajeshi wake katika eneo la Laikipia baadaye mwaka huu, hayatafanyika tena nchini Kenya.

Kutokana na hali hiyo, Uingereza imesema mazoezi hayo yatapelekwa katika nchi nyingine bila ya kutaja ni wapi.

Uingereza haijaeleza ni kwanini haikupata leseni hiyo kutoka kwa serikali ya Kenya, ambapo pia haijatoa sababu.Hatua hata hivyo, haiathiri ushirikino wa kijeshi kati ya Kenya na Uingereza.

London inaendelea kuwa na kambi kubwa ya kijeshi ya kufanyia mazoezi katika eneo la Laikipia inayoitwa BATUK, umbali wa Kilomita 200 kutoka jiji kuu Nairobi.

Baadhi ya wanajeshi wa Uingereza ambao wamekuwa wakifanya mazoezi nchini Kenya kwa miaka mingi, wamedaiwa kuhusika kwenye matukio ya ubakaji wa wenyeji na mauaji, ambapo Kenya imekuwa ikitaka wafunguliwe mashtaka nchini humo, kinyume na msimamo wa Uingereza.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii