Nigeria kuajiri wanajeshi wapya 28,000

Rais wa Nigeria Bola Tinubu ameidhinisha kuajiriwa kwa wanajeshi wapya 28,000 ili kuimarisha ulinzi wa taifa hilo la Afrika Magharibi linaloendelea kukabiliwa na migogoro mbalimbali ya kiusalama.

Katika taarifa iliyotolewa jana, msemaji wake, Bayo Onanuga, alisema kuwa Rais Tinubu ameidhinisha uajiri wa wanajeshi hao wa ziada, akiueleza uamuzi huo kuwa ni hatua muhimu ya kuimarisha mfumo wa usalama wa Nigeria.

Onanuga amesema mpango huo pia unahusisha ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kijeshi pamoja na kuboresha ustawi wa wanajeshi.

Hatua hiyo inakuja wakati serikali ya Nigeria tayari imeanza mchakato wa kuajiri maafisa wapya 50,000 wa polisi ili kuimarisha uwezo wa vyombo vya usalama wa ndani.

Hali ya vurugu nchini Nigeria imeiweka nchi hiyo katika uangalizi mkubwa wa kimataifa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii