EMEDO "Tuungane kubadili muelekeo wa vifo vya kuzama maji"

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya kuzuia kuzama maji duniani jamii jijini mwanza imetakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia usalama wao hasa wanapokuwa katika shughuli za uvuvi ili kuzuia vifo vitokanavyo na kuzama maji.

Rai hiyo imetolewa hii leo na Marry Francis, afisa uchechemuzi  kutoka shirika la usimamizi wa mazingira na maendeleo ya uchumi emedo alipokuwa akizungumza na jembe habari ambapo amesema takwimu za kidunia zinaonyesha kuwa takribani watu zaidi ya laki tatu wanapoteza maisha kutokana na vifo vya kuzama  maji, wazazi wanatakiwa kuwaweka mbali watoto, na  kuwa na uangalizi  wakati wa shughuli zozote  za maji na hasa uvuvi. 

Bi marry amesema kuwa takwimu hizo zilizotolewa na shirika la afya ulimwenguni zinaonyesha kuwa  asilimia 92 ni uchumi wa kati na uchumi mdogo huku asilimia 59 ikiwa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa huku wavuvi wakiwa kwenye hatari kubwa zaidi ya vifo vya kuzama maji

Aidha marry ametoa rai kwa jamii  kuhakikisha inawalinda watoto dhidi ya shughuli mbalimbali zinazohusiana na maji ili kuzuia vifo huku akiwasisitiza watu kuvaa koti okozi muda wote wanapokuwa ndani ya maji pamoja na kufuata taarifa za mamlka ya hali ya hewa  pamoja na kuimarisha vifaa na vyombo vyao vya uvuvi.

Maadhimisho ya siku ya kuzuia kuzama maji hufanyika kila mwaka duniani kote July 25 ambapo kauli mbiu ya mwaka huu 2026. 

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii