Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amekutana na Bw. Massad Boulos, mwanadiplomasia na Mshauri Mwandamizi wa Rais wa Marekani, Donald Trump, anayeshughulikia masuala ya Afrika, nchi za Kiarabu na Mashariki ya Kati.
Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa mkutano wa kimataifa wa Oslo Forum 2026 unaoendelea jijini Oslo, Norway, ukiwakutanisha viongozi, wanadiplomasia waandamizi pamoja na wadau wa amani na usuluhishi kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Mkutano huo unaofanyika kuanzia Juni 10 hadi 12, 2026, unalenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu amani, diplomasia, usuluhishi wa migogoro na namna ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia.
Kukutana kwa Dkt. Kikwete na Massad Boulos kunatajwa kuwa sehemu ya majadiliano yanayolenga kuimarisha uhusiano wa kimataifa na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya amani, maendeleo na ushirikiano kati ya Afrika na washirika wake wa kimataifa.
Dkt. Kikwete ni miongoni mwa viongozi wa Afrika wanaoheshimika kwa mchango wao katika diplomasia, upatanishi na juhudi za kutafuta suluhu za migogoro katika bara la Afrika na maeneo mengine duniani.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime