Idadi ya visa vya Ebola vilivyothibitishwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongezeka hadi 635. Misri imeahidi kuisaidia Kongo katika suala la ebola.
Idadi ya visa vya Ebola vilivyothibitishwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongezeka hadi 635, ikiwa ni pamoja na vifo 127. Idadi hiyo imebainika kwenye data za serikali Jumatano.
Wakati huo huo, wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitangaza ufadhili wa ziada wa dola milioni 20 jana kama sehemu ya kukabiliana na mlipuko wa Ebola barani Afrika.
Wakati haya yakiarifiwa, rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi Jumatano alisisitiza kuiunga mkono Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa ziara ya rais wa Kongo, Felix Tshisekedi huko Cairo.
El-Sissi alisema katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kufuatia mazungumzo akielezea mshikamano wa Misri na Kongo katika kukabiliana na mgogoro wa sasa wa kibinadamu katika sehemu ya mashariki ya nchi na utayari wao wa kutoa aina zote muhimu za msaada wa kimatibabu, chakula na misaada ya kibinadamu katika suala la ebola.