Urusi imesema kuwa inaweza kusitisha operesheni na kuacha kuishambulia Ukraine wakati wowote endapo Ukraine itatimiza masharti ya Urusi
Urusi imeyataja masharti hayo kuwa ni lazima Ukraine iitambue Crimea kama Urusi, na Donetsk na Luhansk kama Mataifa huru.
Urusi pia imesema Ukraine lazima irekebishe katiba yake na kukataa madai ya kuingia katika kambi yoyote kama vile kujiunga na NATO.
Urusi imesema itamaliza vita na kuondoa jeshi Ukraine endapo tu masharti hayo yatatimizwa “Wakitimiza masharti hatua za kijeshi za Urusi zitakoma mara moja”.