Israel na Hezbollah zaendelea kushambuliana

Mapigano yanaendelea kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hezbollah la nchini Lebanon licha kuwepo makubaliano ya kusitisha vita na jitihada za mazungumzo yanayosimamiwa na Marekani.

Jeshi la Israel limesema limefanya mashambulizi makali kusini mwa Lebanon na kuwaua wanamgambo 20 wa kundi hilo lenye mafungamano na Iran katika muda cha saa 24 zilizopita.

Hivyo Hezbollah kwa upande ilifyetua maroketi kuyalenga maeneo ya kaskazini wa Israel Alhamisi jioni na mengi yalidunguliwa huku mengine yalianguka kwenye maeneo ya wazi.

Aidha makabiliano hayo yanaendelea katika wakati maafisa wa Israel na wale wa serikali ya Lebanon wanakutana mjini Washington kwa duru nyingine ya mazungumzo.

Hata hivyo wanalenga kutafuta njia ya kumaliza uhasama pamoja na kulipokonya silaha kundi la Hezbollah lenye ushawishi mkubwa ndani ya Lebanon na ambalo linayapinga mazungumzo hayo.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii