Zelensky ;shambulizi la Urusi limewaua watu 24

Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine amesema leo Ijumaa kuwa shambulizi la Urusi dhidi ya jengo moja la makaazi kwenye mji mkuu Kyiv limewaua watu 24 ikiwemo watoto wa watatu.

Ingawa taarifa hizo amezitoa kupitia ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X akisema idadi hiyo imepatikana baada ya wakoaji kumaliza kufukua kifusi cha jengo hilo lililoshambuliwa jana Alhamisi kwa kombola la masafa.

Aidha kwa mujibu wa Zelensky, mashambulizi ya Urusi kwenye mji huo mkuu yamewajeruhiwa pia watu 48 katika hatua nyingine Urusi na Ukraine zimetangaza kubadilishana mateka wa vita wapatao 205 kwa kila upande.

Hata hivyo mabadilishano hayo tayari yamekamilika na Urusi imetangaza mapema hii leo Ijumaa kuwa imewapokea wanajeshi wake 205 kutoka Ukraine.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii