Trump: Hatuna haraka ya kufikia makubaliano na Iran

Rais wa Marekani amesema kuwa mazungumzo yanaendelea “kwa utaratibu na kwa njia yenye kujenga,” na kusisitiza kuwa hana haraka ya kufikia makubaliano ya kuvimaliza vita baina yake na Iran.

Trump amesema siku ya Mei 24,2026 kupitia mtandao wa Truth Social kwamba licha ya mazungumzo hayo kuendelea lakini hana haraka ya kufikia makubaliano na kuwaagiza wapatanishi wa Marekani kutokimbilia kufikia makubaliano kwa kuwa bado wana muda.

Aidha amesema hayo huku maafisa wa Iran wakieleza kwamba bado kuna vizingiti vikubwa vinavyopaswa kutafutiwa majibu na hususan suala la mali za Iran zinazozuiliwa kwenye mataifa mengine ambazo Tahran inataka ziachiliwe.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii