Spika wa Bunge la Senegal atangaza kujiuzulu

Spika wa Bunge la Senegal ametangaza kwamba atajiuzulu wadhifa huo siku mbili baada ya mshirika wake wa karibu Ousmane Sonko kuvuliwa uwaziri mkuu hatua inayozidisha mzozo wa kisiasa nchini humo.

Ingawa uamuzi huo wa spika El Malick Ndiaye unamfungulia njia Sonko kuwania nafasi hiyo ya kuliongoza bunge linalodhibitiwa na chama chake cha Pastef ili kumkabili Rais Basirou Diomaye Faye.

Aidha mawaziri wamearifiwa kuhudhuria kikao kamili cha bunge siku ya Jumanne asubuhi kumrejeshea ubunge Sonko na kupiga kura ya kumchagua spika mpya imesema sehemu ya waraka rasmi uliochapishwa jana jioni.

Hata hivyo hali hii itazidisha ugumu katik juhudi za mageuzi zilizochukuliwa na Faye aliyemtimua mshirika wake wa awali Sonko siku ya Ijumaa baada ya miezi kadhaa ya mivutano.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii