Mamlaka za nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimesema visa vinavyohisiwa kuwa vya Ebola vimeongezeka na kufikia 900, katikati ya mlipuko wa ugonjwa huo Mashariki mwa taifa hilo.
Hivyo taarifa ya Wizara ya
Mawasiliano iliyochapishwa kwenye mtandao wa X jana Jumapili imesema kulikuwa
na visa 904 na vifo 119 vinavyohisiwa vimetokana na maambukizi ya Ebola.
Hata hivyo mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya ulimwenguni WHO
Tedros Adhanom Gebreyesus amethibitisha takwimu hizo na kuongeza kuwa
juhudi za ufuatiliaji zinazidi kuimarishwa.
Aidha mamlaka za Kongo hapo kabla zilitangaza zaidi ya visa 700 vya Ebola na zaidi ya vifo 170 vilivyoripotiwa zaidi kwenye jimbo la Ituri ambako ndio kitovu cha mlipuko huo.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime