Mlipuko wa virusi vya hanta kwenye meli ya kitalii wazua taharuki huko nchini Argentina huku ikichunguzwa kama chanzo huku abiria wakipelekwa Ulaya kwa matibabu ya dharura.
Maafisa wa afya na wataalamu
nchini Argentina wanahangaika kubaini iwapo nchi hiyo ndiyo chanzo cha mlipuko
hatari wa virusi vya hanta ulioikumba meli ya kitalii katika Bahari ya
Atlantiki.
Dharura hiyo ya kiafya imeibuka wakati Argentina ikishuhudia
ongezeko la maambukizi ya virusi hivyo ambalo watafiti wa afya
wanalihusisha na athari zinazoongezeka za mabadiliko ya tabianchi.
Argentina ambako safari ya meli hiyo kuelekea Antaktika
ilianzia imetajwa mara kwa mara na Shirika la Afya Duniani kuwa miongoni mwa
nchi zenye kiwango kikubwa zaidi cha maambukizi ya ugonjwa huo unaosambazwa na
panya katika kanda ya Amerika ya Kusini.
Aidha abiria wapatao 40 kutoka meli hiyo tayari
wameshuka katika kisiwa cha St. Helena Kusini mwa Bahari ya Atlantiki akiwemo
mke wa raia wa Uholanzi aliyefariki kutokana na mlipuko huo.
Hata hivyo wakati huo huo ndege ya dharura iliyombeba mmoja wa wagonjwa kutoka meli hiyo imewasili Amsterdam nchini Uholanzi huku wagonjwa wengine wawili wakipelekwa Uholanzi na Ujerumani kwa matibabu zaidi.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime