Mkakati wa jeshi la Urusi na kile ilijifunza baada ya kuanguka kwa USSR.

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameelezea uvamizi wa nchi yake dhidi ya Ukraine kama "operesheni maalum ya kijeshi". Lakini, tangu mwanzo, hii haikuwa oparesheni ya kijeshi iliyodhibitiwa na yenye mipaka.

Baadhi wametaja uvamizi huo kama "Operetion Z," baada ya alama za herufi "Z" kuonekana kwenye jeshi la Urusi na magari ya usaidizi.

Na ilikuwa kampeni kubwa na ngumu zaidi ya kijeshi iliyoandaliwa na Moscow tangu uvamizi wa Afghanistan mnamo 1978.

Pia ilikuwa mara ya kwanza ulimwengu ulipata fursa ya kuona uwezo kamili jeshi mpya ya Urusi: jeshi la kisasa lenye utaalamu wa kivita na abalo limeimarishwa kikamilifu tangu vita vya Urusi na Georgia mnamo 2008.


Lakini Urusi ilijifunza nini kijeshi kutokana na mzozo huo, na je, mafunzo hayo yalijidhihirisha katika vita ya sasa huko Ukraine?

Mashambulizi ya sasa ya Urusi yanafanywa na vikosi viwili vipya vya kijeshi "vilivyounganishwa" kutoka wilaya za magharibi na kusini mwa Urusi karibu na mpaka wa Ukraine, ambazo ziliundwa baada ya Urusi kuchukua Crimea mwaka 2014.

Vikosi hivi vimeundwa kutokana na matawi tofauti ya kijeshi - kama vile magari ya kivita, askari wa miguu, makombora na mizinga, usafiri wa anga na uhandisi - na vilipewa kipaumbele katika kampeni ya Kremlin ya kuleta mageuzi katika jeshi.

Wimbi la awali la jeshi la uvamizi wa Urusi lilijumuisha vikundi 60 vya mbinu za kivita (hadi askari 60,000) pamoja na askari wa wenye ujuzi wa hali ya juu angani na vikosi maalum vya operesheni, kitengo cha kutumia silaha za masafa marefu (ambacho huzindua mashambulio ya nyuklia au ya kawaida), na Jeshi la Wanamaji la Urusi.

Kando na hilo, Warusi wametumia wanamgambo kutoka majimbo yaliyojitenga jitenga ya Donetsk na Luhansk, vikosi viwili vya jeshi vinavyojumuisha takriban wanajeshi 40,000, kama kikosi chao kikuu cha mashambulizi mashariki mwa Ukraine.

Sawa na Syria, Warusi pia wanatumia vitengo vya oparesheni maalum kufanya kazi za uchunguzi, kuandaa operesheni za hujuma dhidi ya ''adui'' na kuwalenga viongozi wakuu wa kisiasa na kijeshi, ikiwezekana akiwemo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.

Kingine cha muhimu pia hatua ya Urusi kutumia vitengo maalum vya makomando wa Chechen, maarufu kama "kadyrovtsy".

Kadyrovtsy wanajulikana kuwa wapiganaji hodari, waliozoea vita, na wanaotekeleza majukumu yao bila huruma. Mara nyingu hutumiwa kutia uwoga vikosi vya adui..


Vitengo vya Chechen vimejumuishwa katika opareshini ya kijeshi ya hivi karibuni nje ya nchi, ikiwemo Lebanon, Georgia na Syria.

Mnamo 2014-2015, baadhi ya wapiganaji wa "kujitolea" wa Chechen walipigana kwa ushirikiano na waasi wanaounga mkono Urusi mashariki mwa Ukraine.

Katika vita vya sasa, kadyrovtsy labda itatumika katika shughuli za mijini na wakati wa "upekuzi wa usalama" wa kimfumo ndani ya maeneo yanayokaliwa na Urusi, ambayo bila shaka itasababisha kukamatwa na kuteswa kwa watu wengi.

Awamu ya kwanza ya mashambulio yamelenga miundombini za kijeshi, ikiwemo:

  • msururu wa mashambulio ya makombora na mizing yaliyoratibiwa dhidi ya miundombinu ya kijeshi ya Ukraine (pamoja na viwanja vya ndege, mitambo ya rada, kiengo cha ujasusi wa kijeshi na makao makuu ya kijeshi, maghala ya risasi, mitambo ya kusafisha maji, na mitambo ya jeshi la majini)
  • uvamizi wa kimtandao na vita vya kielektroniki.
  • mashambulizi ya anga ya wakati mmoja na mashambulizi ya vikosi maalum katika maeneo ya mbali ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na kutekwa kwa uwanja muhimu wa kimkakati wa Hostomel nje ya Kiev.
  • mashambulio kutoka upande wa Donetsk na Luhansk yalilenga kushirikisha vikosi vya Ukraine katika mapigano ya muda mrefu ya kujihami
  • kizuizi cha muda dhidi ya miji ya bandari za Ukraine
  • Kuteka miji kadhaa ya Ukraine.


Ingawa Warusi wamekabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa vikosi vya Ukraine, wana faida muhimu katika uwanja wa vita, ikiwa ni pamoja na ubora wa anga na udhibiti wa baadhi ya maeneo ya kimkakati.

Makabiliano ya kijeshi na kusonga mbele kwa wakati mmoja katika nyanja kadhaa pia kumelazimu vikosi vya jeshi laUkraine mashambulizi mara kwa mara na kuzingatia operesheni za ulinzi, haswa katika vituo vikubwa vya mijini.

Mashambulizi ya pande nyingi kwa kutumia mifumo ya kisasa ya mapigano haikuwezekana katika vita vya siku tano vya Urusi na Georgia mnamo 2008.

Ingawa Urusi ilishinda vita haraka, ilipata hasara kubwa.

Mzozo huo ulifichua upungufu wa dhahiri katika vikosi vyake vya kijeshi, ambavyo kwa kiasi kikubwa vilikuwa vua tangu enzi za Muungano wa Kisovieti.

Kwa mfano, wanajeshi wa Urusi hawakutumia zana za hali ya juu au makombora yamasafa marefu katika mzozo huo.

Badala yake, ililazimika kupeleka ndege za kimkakati na kujibu mashambulizi ya angani lakini zilikabiliwa na ulinzi mkali wa anga wa Georgia, ambao ulidungua ndege kadhaa za Urusi

Nchini Ukraine, Urusi sasa inategemea mashambulizi ya makombora ya masafa marefu, yenye ubora wa hali ya juu, kutoka angani, baharini na nchi kavu, ambao umepunguza hatari ya ndege za Urusi kudunguliwa.

Huko Georgia, mizinga ya zamani ya Urusi na magari mengine ya kivita yaliingia katika maeneo makubwa ya mijini na kulazimishwa kushiriki katika mapigano ya muda mrefu ya mitaani.

Huko Ukraine, vikosi vya Urusi hapo awali viliazimia kuzingiraa miji mikubwa katika jaribio la kushinikiza jeshi la Ukraine kujisalimisha.

Lakini mkakati huo haukufikia malengo yake kwani vikosi vya Ukraine viliwadhibiti wavamizi hao wa Urusi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii