Kiongozi wa Hezbollah apinga Lebanon na Israel kuzungumza

Kiongozi wa kundi la Hezbollah la nchini Lebanon, Naeem Qassem, ametoa mwito wa kufutuliwa mbali mazungumzo ya nadra na moja kwa moja kati ya Lebanon na Israel yanayotazamiwa kuanza leo mjini Washington, Marekani.

Kupitia hotuba aloitoa kwa njia ya televisheni, Qassem, ameirai serikali mjini Beirut kuchukua "msimamo wa kihistoria" kwa kuachana na mipango ya kuzungumza na Israel akisema "mwelekeo huo siyo sahihi" kwa taifa hilo.

Israel imekuwa ikiishambulia Lebanon kwa malengo ya kulitokomeza kundi la Hezbollah lenye mafungamano na Iran, ambalo lilijiunga na vita dhidi ya Iran kwa dhamira ya kuisaidia serikali ya Tehran.

Baada ya shinikizo kubwa, Israel ilitangaza wiki iliyopita kuwa tayari kufanya mazungumzo na Lebanon kwa dhamira ya kulipokonya silaha kundi la Hezbollah na kuimarisha mahusiano ya amani baina ya mataifa hayo jirani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii