Safari ya kurudi Mwezini kwa binadamu kupitia mpango wa NASA inaendelea kuvutia hisia za dunia hasa kupitia misheni ya Artemis II ambayo ni hatua muhimu kabla ya kutua tena Mwezini.
Hata hivyo pamoja na mafanikio ya kisayansi yanayotarajiwa, suala la gharama limekuwa likiibua maswali mengi: je, maandalizi haya ya kihistoria yanagharimu kiasi gani?
Gharama Kubwa ya Programu ya Artemis
Mpango mzima wa Artemis unatajwa kuwa miongoni mwa miradi ya gharama kubwa zaidi katika historia ya anga kwa mujibu wa makadirio ya NASA na wachambuzi wa anga, gharama ya jumla ya programu hii inaweza kufikia zaidi ya dola bilioni 90 za Marekani (Sawa na Sh Trilioni 234), ikijumuisha utafiti, ujenzi wa teknolojia na misheni mbalimbali.
Programu hii haijajikita katika safari moja tu, bali ni mkakati wa muda mrefu wa kurejesha uwepo wa binadamu Mwezini na baadaye kuelekea sayari ya Mars.

Roketi na Teknolojia ya Uzinduzi
Kipengele muhimu katika misheni ya Space Launch System (SLS) ndicho kinachobeba gharama kubwa zaidi katika kila safari. Roketi moja ya SLS inakadiriwa kugharimu kati ya dola bilioni 2 hadi 4, kutokana na teknolojia yake ya hali ya juu na mahitaji ya usalama wa juu sana.
Roketi hii ndiyo itakayobeba wanaanga na chombo cha Orion kuelekea anga ya mbali zaidi ya Dunia.
Chombo cha Wanaanga: Orion Spacecraft
Chombo cha Orion spacecraft ndicho kitakachowabeba wanaanga wa Artemis II katika safari yao ya kuzunguka Mwezi. Maendeleo ya chombo hiki pekee yamegharimu zaidi ya dola bilioni 20 kwa miaka ya utafiti na ujenzi.

Orion imeundwa kwa viwango vya juu vya usalama, ikiwa na uwezo wa kustahimili safari ndefu za anga na kurudi salama duniani.
Ingawa gharama za kila sehemu zimegawanyika ndani ya programu kubwa ya Artemis, makadirio yanaonyesha kuwa misheni ya Artemis II pekee inaweza kugharimu kati ya:
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii