DKT. ABBAS: UHIFADHI UMEIFANYA TANZANIA KUONGOZA KWA SIMBA WENGI DUNIANI

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Utalii, Wanyamapori na Malikale ya UGANDA Bi. Doreen S. Katusiime ambaye yupo nchini Tanzania na timu yake kufanya ziara ya mafunzo kuhusu namna Tanzania inavyokabiliana na ujangili na biashara haramu ya nyara. 

Katika ziara hiyo timu ya Uganda inatembelea Mradi wa Kupambana na Ujangili na biashara haramu ya nyara ikiwa ni mpango maalumu wa ziara za mafunzo baina ya nchi zinazotekeleza Miradi yenye malengo yanayoshabihiana ili kubailishana uzoefu nakujifunza namna nchi nyingine inavyotekeleza Mradi wake.

Akizungumzia mafanikio ya Uhifadhi nchini Dkt. Abbasi alieleza kuwa ni pamoja kupunguzwa ujangili kwa kiasi kikubwa ambapo leo Tanzania inaongoza duniani kwa kuwa na simba wengi wapatao 17,000. Uganda inao 6,500 pekee.

Viongozi hao wamekubaliana kuendeleza ushirikiano baina ya sekta wanazozisimamia ili ziwe na mchango zaidi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii