Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) imelaani vikali kitendo kinachodaiwa kufanywa na Madam Rita dhidi ya chombo cha habari cha mtandaoni, ikikitaja kuwa ni kinyume na maadili ya taaluma ya habari.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa JUMIKITA, Dickson Mushi, kwa niaba ya Mwenyekiti Shaban Matwebe, jumuiya hiyo imesema tukio hilo linaonesha dharau, ukosefu wa adabu na kutoheshimu vyombo vya habari pamoja na wanahabari kwa ujumla.
JUMIKITA imeeleza kuwa taaluma ya habari inapaswa kulindwa na kuheshimiwa na wadau wote bila kujali nafasi au hadhi ya mtu katika jamii, na kusisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili katika utoaji na ushirikiano wa habari.
Kutokana na tukio hilo, jumuiya hiyo imetoa wito kwa vyombo vyote vya habari nchini kusitisha kumpa ushirikiano Madam Rita hadi pale atakapojitokeza hadharani kuomba radhi kwa umma pamoja na chombo cha habari kilichoathirika.
JUMIKITA imeeleza kuwa hatua hiyo inalenga kulinda heshima na misingi ya taaluma ya habari nchini.

10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime