Papa Leo aelekea Saurimo Angola kwa ibada ya misa

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV, amesafiri mapema leo kuelekea mjini Saurimo mashariki mwa Angola kutoka mji mkuu Luanda, kwa mfululizo wa hafla za kidini, kama sehemu ya ziara yake nchini humo.

Mjini Saurimo, papa anatarajiwa kuzuru makazi ya wazee kabla ya kuongoza Misa Takatifu katika eneo moja la wazi mjini humo.

Baada ya misa,  Papa Leo atarejea Luanda saa za alasiri ambako anatarajiwa kuhitimisha siku yake kwa kukutana na maaskofu, wahudumu katika Parokia ya Our Lady of Fatima na kuhutubia.

Jana Jumapili, akiongoza maombi katika eneo takatifu la Mama Muxima,kiongozi huyo wa kiroho, alikumbuka "huzuni na mateso makubwa” waliopitia watu wa  Angola kwa karne nyingi.

Akiwahutubia takriban waumini 30,000 waliojitokeza katika eneo hilo, Papa Leo aliwahimiza kujenga ulimwengu bora zaidi ambapo hakutakuwa tena na vita , dhulma, umaskini wala udanganyifu.

Papa Leo anatarajiwa kuondoka Angola kesho na kuelekea Guinea ya Ikweta atakapokamilisha ziara yake ya siku 11 katika nchi nne za Afrika.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii