Wagombea wanne wa wadhifa wa katibu mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa watafika wiki hii mbele ya jopo la mabalozi kutoka nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa mahojiano ya kazi.
Kesho Jumanne, rais wa zamani
wa Chile Michelle Bachelet, mmoja kati ya wanawake wawili na raia watatu wa
Amerika ya Kusini, atakuwa wa kwanza kufika mbele ya jopo hilo la mahojiano
wakati wa kikao cha masaa matatu .
Bachelet atafuatwa na mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti
Nguvu za Atomiki, IAEA, Rafael Mariano Grossi kutoka Argentina.
Siku ya Jumatano, itakuwa zamu ya mkuu wa masuala ya kibiashara
wa Umoja wa Mataifa Rebeca Grynspan na hatimaye, Rais wa zamani wa Senegal Macky Sall.
Wakati wa vikao hivyo, wagombea hao wanne wanatarajiwa kuhojiwa kuhusu maono yao kwa kazi hiyo,maeneo tete ya duniani na mustakabali wa Umoja wa Mataifa miongoni mwa masuala mengine.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime