AU yalaani hatua ya Israel kumteua balozi mpya Somaliland

Umoja wa Afrika hapo jana "ulilaani vikali" hatua ya Israel kuteua balozi mpya kwenye eneo la Somaliland linalotaka kujitenga na Somalia, uamuzi iliyosema ni kuingilia uhuru wa Somalia.

Katika taarifa iliyotolewa hapo jana, umoja huo ulieleza kuguswa na hatua ya Israel na kusisitiza uungaji mkono wake kwa serikali ya Mogadishu.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, AU haitambui Somaliland kama nchi huru na kwamba uamuzi wowote wa kujaribu kuingilia uhuru wa kujitawala wa Somalia ni batili na haukubaliki.

Desemba 26 mwaka jana nchi ya Israel ilikuwa taifa la kwanza duniani kuitambua Somaliland kama nchi huru, tangazo lililosababisha ukosoaji toka kwa serikali ya Mogadishu na Jumuiya ya kimataifa.

Katika mkutano wa ngazi ya mawaziri uliofanyika Januari 6, Baraza la Amani na Usalama la AU lilikataa kutambuliwa kwa Somaliland kama nchi, na kutaka hatua hiyo kubatilishwa.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii