Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Leo wa 14, amekemea vitendo vya rushwa na kuzitaka mamlaka za Angola kumaliza ubaguzi ambao umeendelea kusumbua nchi hiyo tangu kumalizika kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002, kauli aliyotoa wakati alipoongoza misa iliyohudhuriwa na waumini zaidi ya laki moja kwenye mji wa Kilaba.
Papa Leo aliwasili katika taifa hilo lenye utajiri wa rasilimali wikendi iliopita, ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mataifa manne ya bara ya Afrika.
Katika ziara hiyo, Papa amelaani hatua ya mataifa tajiri kuendelea kuiba rasilimali za Bara Afrika.
Angola ni mojawapo wa mataifa ya Afrika yenye utajiri wa mafuta na madini ya almasi lakini licha ya utajiri huo, raia wake zaidi ya Milioni 36 wanaishi katika umaskini kwa mujibu wa takwimu za benki ya dunia.
Hii leo Papa anatarajiwa kuzuru Mji wa Saurimo ulioko kilomita 800 kutoka Mji Mkuu wa Angola Luanda, Mji ambao unaelezwa kuwa wakazi wake wametengwa na una utajiri wa madini ya Almasi.
Papa Leo baadae hivi leo anatarajiwa kuelekea nchini Equatorial Guinea atakapohitimishia ziara yake ya siku 11 barani Afrika.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime