Bayern Munich yatwaa ubingwa wa 35 wa Bundesliga

Bayern Munich ndio mabingwa wa ligi kuu ya Ujerumani "Bundesliga" msimu huu, baada ya kupata ushindi siku ya Jumapili wa mabao 4-2 dhidi ya Stuttgart na hivyo kulichukua taji hilo la 35.

Ushindi huo umewafanya Bayern kuwa mbele kwa alama 15 dhidi ya Borussia Dortmund walio katika nafasi ya pili japo wamesalia na michezo minne.

Bayern walipoteza mchezo mmoja tu katika ligi msimu huu, walipochuana wakiwa nyumbani dhidi ya Augsburg mwezi Januari, huku wakitoka sare katika mechi nne hadi sasa na  kufunga jumla ya mabao 109, hii ikiwa ni rekodi nyingine.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii