Pakistan yapendekeza duru ya pili ya mazungumzo

Marekani imeweka mzingiro katika bandari za Iran kuzuia meli, wakati Pakistan ikipendekeza mazungumzo mengine kumaliza vita vinavyoendelea.


Maafisa wa Pakistan wamefahamisha kwamba nchi hiyo imependekeza duru ya pili ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran kumaliza vita inayoendelea.

Pendekezo la Islamabad limetolewa wakati Marekani ikiweka vizuizi kamili leo katika bandari za Iran, huku Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance akisema mazungumzo na Iran yamepiga hatua na Rais Donald Trump akionesha jana Jumatatu kwamba Iran iko tayari kufikia makubaliano.

Pakistan yapendekeza awamu nyingine ya majadiliano ya usuluhishi kati ya Iran na Marekani

Kwa upande mwingine, jana afisa mmoja mwandamizi wa kundi la Hezbollah alisema kundi hilo halitozingatia makubaliano ya aina yoyote ambayo yatatokana na mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Lebanon na Israel yatakayoanza leo huko Washington.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii