MBUNGE wa Jimbo la Lupembe, Edwin Swalle ameishauri serikali kuleta bungeni sheria ya mikopo ya asilimia 10 ili kufanyiwa marekebisho.
Amependekeza hatua hiyo ili kuwe na ruhusa mtu mmoja mmoja kunufaika na mikopo hiyo. Akisema anaamini hatua hiyo itasaidia kupunguza changamoto ya kutorejeshwa kwa mikopo hiyo.
Swalle ametoa kauli hiyo leo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
“Marekebisho hayo yatawapa fursa watu wenye mawazo ya biashara au wanaoendesha biashara zao kupata mikopo na kuirejesha kwa wakati, jambo litakalosaidia kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kuongeza ajira na tija kwa wananchi,” amesema.Aidha, ameishauri serikali kuchukua hatua kudhibiti ongezeko la bidhaa feki mitaani, ikiwemo pombe bandia.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime