Waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dkt. Mwigulu Nchemba leo Aprili 13, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo rasmi na Balozi wa Slovakia nchini Tanzania, Ivan Lancaric.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za Bunge zilizopo jijini Dodoma, yakilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili.
Aidha katika kikao hicho, pande zote mbili zimejadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo uwekezaji, biashara na fursa za maendeleo zinazoweza kuwanufaisha wananchi wa Tanzania na Slovakia.
Hata hivyo mazungumzo haya yanaendelea kuonesha juhudi za Tanzania za kuimarisha diplomasia ya kimataifa na kuvutia washirika wapya wa maendeleo katika sekta mbalimbali za uchumi.

10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime