Kiongozi huyo wa juu zaidi wa kanisa katoliki duniani anaendelea na ziara yake barani Afrika akiwa katika siku ya pili katika kituo chake cha kwanza cha ziara hiyo nchini Algeria.
Kiongozi mkuu wa Kanisa
Katoliki duniani Papa Leo wa XIV ametowa mwito wa amani na kumalizwa kwa tabia
ya ukoloni mamboleo inayoendelea duniani.
Matamshi hayo ya papa aliyatowa mwanzoni mwa ziara yake nchini
Algeria jana na kuandamwa na kauli za kushambuliwa vikali kwa maneno na Rais
Donald Trump na makamu wake JD Vance, baada ya kukosoa vita vya Marekani na
Israel dhidi ya Iran.
Papa Leo XIV kufanya ziara mjini Annaba nchini Algeria
Aidha hivi leo kiongozi huyo wa kiroho anatarajiwa katika mji wa
Annaba ambako atatembea kufuata nyayo za Mtakatifu Augustino, mwanatheolojia
aliyekuwa na taathira kubwa katika Ukristo ambapo ataendesha misa katika kanisa kubwa
la Mtakatifu Augustino mbele ya viongozi wa kanisa hilo kutoka barani Afrika.
Itakumbukwa kuwa Papa Leo ni kiongozi wa kwanza wa juu wa Kanisa Katoliki duniani kuitembelea Algeria, ambacho ni kituo cha kwanza cha ziara yake ya mataifa manne ya Afrika.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime