SERIKALI ya Ukraine wamethibitisha kuwa wanajeshi wasiopungua 70 waliuawa katika shambulio la makombora ya Urusi katika kambi yao ya kijeshi juzi Jumapili, Februari 27, 2022.
Shambulio hilo lilitokea Okhtyrka, katika eneo la Sumy ambalo kwa sasa limezingirwa na majeshi ya Urusi. Mpaka jJana, Jumatatu, kikosi cha dharura kilikuwa bado kikipekua vifusi kujaribu kutafuta manusura wa kombora hilo.
Hivi punde, Bunge la Ukraine limetoa taarifa rasmi ya kuwaenzi wanajeshi hao, likisema wanajeshi hao waliuawa na makombora ya Grad. “Utukufu wa milele kwa mashujaa wa Ukraine…,” limesema Bunge.