Chama
cha Kijani kimetoa wito kwa serikali kufafanua sheria inayowataka wanaume raia
wa Ujerumani wenye umri kati ya miaka 17 na 45 kupata idhini kutoka kwa jeshi
ili kukaa kwa zaidi ya miezi mitatu nje ya nchi.
Chama cha Kijani cha Ujerumani
kimetoa wito kwa serikali kufafanua
sheria inayowataka wanaume raia wa Ujerumani wenye umri kati ya miaka 17 na 45
kupata idhini kutoka kwa jeshi ili kukaa kwa zaidi ya miezi mitatu nje ya nchi.
Sara Nanni, msemaji wa sera za usalama wa chama hicho,
ameliambia gazeti la Die Welt kwamba
raia wa Ujerumani wanayo haki ya kujua haraka kama wanatakiwa kuripoti, na
ikiwa ni hivyo, wafahamishwe wajibu wao wa kuripoti.
Sheria hii ni sehemu ya sheria mpya ya huduma za kijeshi ya
Ujerumani, ambayo ilianza kutumika Januari mosi. Hata hivyo, kipengele
hiki kilikuwa kimepuuzwa sana kabla kumulikwa zaidi na ripoti za vyombo vya
habari katika siku za hivi karibuni.
Kwa upande wake msemaji wa wizara ya ulinzi ya Ujerumani alinukuliwa
akisema kwamba tayari wizara hiyo ilikuwa imeshathibitisha kanuni hiyo tangu kutangazwa kwake.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime