Kamandi ya jeshi la Iran, imeonya kuwa kutakuwa na madhara zaidi kwa mataifa jirani ikiwa Marekani na Israel zitashambulia miundombinu yake ya nishati na raia.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la mapinduzi la Iran, Khatam al-Anbiya, ikiwa miundombinu yake itashambuliwa kwa mara nyingine, nchi hiyo itajibu vikali mashambulio hayo ambaye amesema kwa upande wao hawatachagua.
Onyo la Tehran, linakuja saa chache kupita tangu rais Donald Trump, atoe makataa ya hadi kesho usiku kwa Iran kuwa imefungua mlango Bahari wa Hormuzi, ama vinginevyo ijiandae kwa mashambulio makubwa zaidi kuwahi kufanywa.
Trump alitoa kauli hii wakati alipokuwa akithibitisha jeshi la nchi yake kufanikiwa kumuokoa rubani wa pili ambae ndege yao ya kivita ilidunguliwa katika milima ya Iran, na kusababisha operesheni kubwa zaidi ya uokozi kuwahi kufanywa na Marekani.
Licha ya Washington kudai imeharibu kwa zaidi ya asilimia 90 miundombinu ya kijeshi ya Iran, Tehran bado imeonesha kuwa inauwezo wa kujibu mashambulio hayo, hali inayoibua maswali kuhusu tambo za Marekani.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime