Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Emmanuel Nchimbi, amekutana na kusalimiana na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Pope Leo XIV, mara baada ya kushiriki Ibada ya Hija iliyofanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Vatican.
Tukio hilo limefanyika Aprili 1, 2026 katika eneo la St. Peter’s Basilica, moja ya maeneo matakatifu na muhimu zaidi kwa waumini wa Kanisa Katoliki duniani.

Katika hafla hiyo ya kiroho viongozi hao wawili walipata fursa ya kusalimiana na kubadilishana salamu tukio linaloashiria uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Kanisa Katoliki duniani.
Ibada hiyo ya hija imehudhuriwa na maelfu ya waumini kutoka mataifa mbalimbali waliokusanyika Vatican kwa ajili ya maombi na ibada maalum ikiwa ni sehemu ya ratiba ya matukio ya kidini yanayofanyika katika makao makuu ya Kanisa Katoliki.
Ushiriki wa Makamu wa Rais katika ibada hiyo unaonesha umuhimu wa diplomasia ya kidini pamoja na mshikamano wa kimataifa katika masuala ya imani na maadili.

10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime