• Jumatano , Januari 22 , 2025

Mganga anatafutwa kwa ubakaji

Polisi Mkoani Lindi wanamtafuta Juma Salumu maarufu ‘Juma kipanya’ ambaye ni mganga wa kienyeji mkazi wa Manispaa ya Lindi kwa tuhuma za kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 15 Wilayani Lindi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Foka Dinya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa Mama Mzazi wa Mtoto huyo aligundua Mtoto wake kuwa mjamzitp mwezi Disemba 2021 na alitoa taarifa Polisi Februari 3, 2022 ambapo tayari Mganga huyo alikuwa ametorokea kusipojulikana.

Kwa upande wake Mama Mzazi wa Mtoto huyo amesema mwezi wa sita mwaka jana Mtoto wake alipelekwa kwa Mganga huyo na Babu yake kwa madai ya kwenda kutengeneza dawa baada ya Mganga kutoa sharti la dawa yake ni lazima itengenezwe na Binti kigoli (asiyezaa wala kushiriki tendo la ndoa) na alipopelekwa Binti huyo alimbaka kisha kumtishia asiseme kwa Watu kwani akisema mizimu itampa adhabu.

Mama huyo amesema Binti yake aliporudi nyumbani hakusema chochote na aliendelea na masomo yake mpaka ilipofika December 2021 ambapo waligundua hali isiyokuwa ya kawaida na walipombana akaeleza kwamba alibakwa na mganga Juma Salum alipokwenda kutengeneza dawa ya Babu yake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii