Rais Emmanuel Macron kukitembelea kisiwa cha Cyprus

Ofisi ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron imesema atakutana na mwenzake wa Cyprus Nikos Christodoulides na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis huko Paphos kuonyesha mshikamano na hatua za kina za kuimarisha usalama kuzunguka Cyprus na mashariki mwa Mediterania.

Ikulu ya Elysee ilisema hapo jana kwamba ziara hiyo itafanyika huku vita vya Marekani na Israeli dhidi ya Iran vikiingia wiki yake ya pili, na kuathiri sehemu kubwa ya Mashariki ya Kati.

Cyprus ililengwa wiki iliyopita na ndege zisizo na rubani zilizotengenezwa Iran, na kumfanya Macron kuagiza meli ya kubeba ndege ya Charles de Gaulle ya Ufaransa kwenda Mediterania na vitengo vya ulinzi wa anga na ndege kwenda Cyprus.

Elysee ilisema ziara ya Macron inakusudiwa kuonyesha mshikamano wa Ufaransa na Cyprus, nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya ambayo tuna ushirikiano wa kimkakati nayo" na ambayo hivi karibuni ilikumbwa na droni kadhaa na mashambulizi ya makombora.

Macron alisema baadaye alikuwa amezungumza na wenzake wa Marekani na Iran Jumapili kabla ya safari hiyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii