Iran yaishambulia Israel kufuatia uteuzi wa Ayatollah Seyyed

Iran imerusha makombora yake ya kwanza kuelekea Israeli Jumatatu baada ya kuteuliwa kwa kiongozi mpya mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu, Ayatollah Seyyed Mojtaba Khamenei.

Kituo cha utangazaji cha serikali IRIB kimesema kwenye chaneli yake ya Telegram kwamba Iran imevurumisha wimbi la kwanza la makombora chini ya Ayatollah Mojtaba Khamenei kuelekea maeneo yaliyokaliwa.

Imechapisha picha ya kombora lenye kauli mbiu "Kwa Amri Yako, Sayyid Mojtaba," marejeleo ya kidini ya madhehebu ya Kishia.

Wakati haya yakiarifiwa, waziri Mkuu wa Qatar na waziri wa mambo ya nje Mohammed bin Abdulrahman Al Thani ametoa wito wa kupunguzwa kwa kiwango cha vita vya Iran.

Akizungumza na Sky News Al Thani amesema hawakutarajia mashambulizi ya jirani yao Iran dhidi ya nchi za Ghuba, akiongeza kwamba uhalali na visingizio vya Tehran wanavyotumia vimekataliwa kabisa.

Wakati huo huo shambulizi la droni lililofanyw ana Iran nchini Bahrain limewajeruhi raia 32 katika kisiwa cha Sitre.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii