Tume ya kuchagua kiongozi mkuu mpya wa Iran imetangaza leo Jumapili, Machi 8, kuwa imefikia uamuzi wa kumchagua kiongozi mpya wa nchi hiyo, ingawa jina la kiongozi huyo bado halijawekwa wazi hadharani.
Uteuzi huo unakuja kufuatia kifo cha aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei, aliyeripotiwa kufariki dunia Februari 28, 2026 baada ya shambulio la pamoja la United States na Israel.
Kwa mujibu wa mwanachama wa tume hiyo anayewakilisha Mkoa wa Khuzestan, Mohsen Heydari, mgombea anayefaa zaidi tayari amechaguliwa baada ya kupitishwa na wingi wa kura katika baraza la wataalamu. Alitoa taarifa hiyo kupitia Iranian Students News Agency (ISNA).
Aidha, mwanachama mwingine wa baraza hilo, Mohammad Mehdi Mirbagheri, pia amethibitisha kupitia video iliyoripotiwa na Fars News Agency kuwa uamuzi thabiti unaoakisi maoni ya wengi tayari umefikiwa.