Aliyejiteka Kenya akamatwa

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) imemtia nguvuni Waziri wa zamani Nchini Kenya, Raphael Tuju ambaye Familia yake ilidai ametekwa kabla ya kujitokeza na kukiri kuwa mafichoni siku ya Jumamosi baada ya kuhisi kuwa kuna Watu walikuwa wakimfuata.

Akizungumza baada ya Tuju kuonekana akiwa ndani ya Nyumba yake Kaumbu, Mkurugenzi wa DCI, Amin Mohamed, amesema uchunguzi wa kina wa kuthibitisha kuonyesha kwamba madai yake yalikosa ukweli.

Amin amesema kuwa Tuju alikuwa amejificha ndani ya Makazi yake muda wote wa kutoonekana kwake, huku timu ya uchunguzi ikituma uchunguzi maalumu baada ya taarifa ya kutoweka kwake kuwasilishwa Jumamosi.

Aidha, taarifa zinasema kuwa Waziri Tuju alifanya hivyo kutokana na kwamba alishindwa kulipa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki, na sasa Benki hiyo inataka kuchukua mali zake, Tuju akituhumu baadhi ya Watu Mashuhuri Serikalini kwa kuhusika kwenye mzozo huo.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii