Rais wa Marekani Donald Trump amewaambia waandishi wa habari akiwa Palm Beach kwamba Marekani na Iran zina maeneo makubwa ya makubaliano katika mazungumzo yao yanayoendelea.
Akiwa karibu na ndege ya Air Force One, Trump alisema mazungumzo hayo yamekuwa yenye nguvu sana, akibainisha kuwa washauri wake, akiwemo Steve Witkoff pamoja na mkwe wake Jared Kushner, wamehusika katika mchakato huo wa majadiliano.
Trump alisema Marekani imekuwa ikizungumza na mtu wa juu kutoka upande wa Iran, ingawa si kiongozi mkuu mpya, na akaongeza kuwa: “Hatujui kama yuko hai.”
Alisisitiza kuwa mazungumzo yanaendelea na bado yatafahamika mwelekeo wake, huku akisema kuna uwezekano mkubwa wa makubaliano katika maeneo mengi.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime