Punguzo kubwa la misaada laongeza hali mbaya nchini Kongo

Umoja wa mataifa siku ya jumatatu umeonya vikali kuhusu kitisho kinachowakabili zaidi ya watu milioni 4 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na ufadhili wa kiutu kupunguzwa kwa kiasi kikubwa.

Kufuatia kitisho hicho, Shirika la Misaada ya kiutu la Umoja huo, OCHA limelizindua "ombi la dharura" la dola bilioni 1.4 kusaidia operesheni zake za mwaka 2026 nchini humo, ambako kunashuhudiwa janga la kibinadamu lililodumu kwa muda mrefu lakini linapuuzwa.

Kwa mwaka huu wa 2026, OCHA litajikita katika kuwasaidia watu milioni 7.3, tofauti na milioni 11 waliopewa kipaumbele mwaka uliopita, imesema taarifa, hii ikiwa ni kutokana na kupungua kwa ufadhili.

Mwaka 2025, watu milioni 1.5 hawakuweza kupata huduma za msingi za afya baada ya vituo kufungwa, upungufu wa dawa muhimu na uwezo mdogo wa kukabiliana na majanga, OCHA limesema.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii