Vifo na majeruhi wa Urusi na Ukraine huenda wakafika mil.2

Idadi ya wanajeshi wa Urusi na Ukraine waliokufa, kujeruhiwa ama kupotea maisha  huenda ikafikia milioni 2 katika majira ya machipuko huku Urusi ikiwa imeathirika zaidi tangu Vita vya Pili vya Dunia.

Katika ripoti ya Kituo cha Masomo ya Kimkakati na Kimataifa, CSIS iliyochapishwa siku ya Jumanne imesema watu milioni 1.2 wa Urusi walikufa ama kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wanajeshi 325,000 waliokufa katika kipindi cha kati ya Februari 2022 na disemba 2025.

Ripoti hiyo inakadiria kwamba watu 500,000 hadi 600,000 walikufa ama kujeruhiwa nchini Ukraine ambako kuna raia na wanajeshi wachache, miongoni mwao waliokufa ni 140,000.

Hata hivyo takwimu hizo zimechapishwa chini ya mwezi mmoja wa maadhimisho ya miaka minne tangu Urusi ilipoivamia kikamilifu Ukraine tangu Februari, 2024.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii