Lishe sahihi ina mchango mkubwa katika kulinda na kuboresha afya ya figo. Kwa mujibu wa wataalamu wa lishe, uchaguzi wa matunda sahihi unaweza kusaidia kupunguza mzigo kwa figo hasa kwa watu wenye matatizo ya figo au wanaoishi na ugonjwa wa figo sugu (CKD).
Akizungumza kuhusu umuhimu wa lishe Dkt. Dao Thi Yen Thuy Mkuu wa Idara ya Lishe na Dietetics katika Hospitali ya Tam Anh, Ho Chi Minh City, anasema wagonjwa wa figo wanapaswa kudhibiti kwa makini ulaji wa potasiamu, sodiamu na fosforasi, kwani madini haya yakizidi huongeza kazi nzito kwa figo.
Aidha, anashauri kula matunda yenye antioxidants na nyuzinyuzi (fiber) kwa wingi.
nye maji mengi na rahisi kumeng’enywa. Yana potasiamu kidogo na yana nyuzinyuzi, vitamini C na antioxidants zinazosaidia mmeng’enyo wa chakula, afya ya moyo na kulinda seli za figo.
Ushauri wa Daktari
Dkt. Thuy anashauri wagonjwa wa figo:
Kuepuka au kupunguza matunda yenye potasiamu nyingi kama ndizi, machungwa, maembe yaliyoiva, parachichi na viazi vitamu
Kupunguza matumizi ya chumvi na viungo vikali
Kuepuka vyakula vya viwandani na vyenye chumvi nyingi
Kugawa chakula katika milo midogo midogo ili kupunguza mzigo kwa figo
Pia, wagonjwa wanashauriwa kunywa maji kwa kiwango kinachopendekezwa na daktari kulingana na hali yao ya afya, kwani maji mengi au machache kupita kiasi yanaweza kuathiri figo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime