Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya mapenzi kikamilifu au kushindwa kusimamisha via ya uzazi kwa mwanaume katika shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili, homoni, neva, hisia na mishipa ya damu, misuli ya uume.ufu wa nguvu za kiume.
Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kutokuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalohitaji tiba. Wanaume wenye changamoto hii mara zote wanahitaji dawa zisizo na madhara au virutubisho tu kutokana na lishe ya mchanganyiko wa vyakula vya vinavyotokanana na mimea na matunda na kubadilisha mitindo ya kimaisha ili kuweza kurudisha hali zao na kuondoa tatizo.
Kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika unaposimama, hutakiwa kuwa imara kama mti mkavu lakini kwa mwanaume mwenye changamoto ya upungufu za nguvu za kiume uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na unaweza kusinyaa wakati wowote.
Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume ambayo ndio huufanya uume usimame barabara. Mwanaume mwenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume akishakamilisha mshindo mmoja wa tendo la ndoa basi anakua hana uwezo tena wa kurudia mshindo mwingine
Zifuatazo ni baadhi ya sababu za upungufu wa nguvu za kiume;
1.Matatizo Ya Kiafya.
Matatizi ya kiafya ya muda mrefu (chronic diseases) husababisha kupungua kwa matatizo ya hamu ya kufanya tendo la ndoa mfano tatizo la kisukari, tatizo la presha, tatizo la moyo, tatizo la kansa ya muda mrefu, na hali ya kuwa na unene uliozidi kiwango (obesity) n.k
2. Msongo Wa Mawazo (Depression).
Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa kisaikolojia unaohusisha hali ya kuwa na mawazo makali kwa muda mrefu yanasababisha kukosa raha kutokana na kujihisi si mtu wa thamani au kukosa starehe katika vitu ulivyozoea kuvifanya na kukufurahisha hapo awali. Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha yako ikiwa ni pamoja na kukosa matamanio ya kimapenzi.
3. Matumizi Ya Madawa Na Pombe.
Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji wa pombe wa kupindukia vinaweza kusababisha tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Madawa yanayochangia tatizo hili ni pamoja na; Madawa ya presha ya kupanda (Anti hypertensive drugs), madawa ya kuondoa msongo wa mawazo, madawa yote yanayozuia ufanyaji kazi au uzalishaji wa testosterone kwa mfano cimetidine, finasteride na cyproterone n.k
4. Mawazo/Uchovu.
Matatizo ya kikazi na hadhi yako kazini vinaweza kuchangia kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.Kama unabezwa sana kazini na kujiona hutimizi kazi yako ipasavyo au kama unachoka sana kazini pia vinaweza kusababisha kukosa hamu ya kufanya mapenzi pindi urudipo nyumbani.
5. Umri Mkubwa.
Kiwango cha homoni ya testosterone inayohusika na hisia za kimapenzi kwa mwanaume hupungua kwa asilimia moja mpaka mbili kila mwaka kadri mwanaume anavyozidi kuwa na umri mkubwa.
Kiwango cha testosterone kikishuka katika mwili wa mwanaume humfanya asiwe na nguvu za kiume, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi.
6. Ugomvi wa mwanaume na mwanamke
Ugomvi au mvurugano wa kimahusiano kati ya mwanaume na mwanamke yana mchango mkubwa sana katika kusababisha tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, mfano ukosefu wa amani na furaha katika mahusiano huchangia sana mwanaume kukosa hamu ya kufanya mapenzi.
Kuwahi kufika kileleni ni tatizo n ani hali ambayo inampata mwanaume mwenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume ambapo hutoa manii kabla ya kuanza tendo la ndoa au muda mfupi tu baada ya kuanza tendo la ndoa bila yeye mwenyewe kukusudia.
Aidha kwa kawaida mtu mwenye tatizo la kuwahi kufika kileleni hutoa mbegu zake za kiume hata baada ya maandalizi kidogo sana.
Kwa kawaida mwanaume anatakiwa afike kileleni/kutoa manii kwa muda usiozidi dakika 30 wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Hata hivyo mwanaume anaposhiriki tendo la ndoa na kuchukua muda mrefu bila kufika kileleni anahitaji uchunguzi ili kubaini chanzo cha tatizo na endapo ukiona dalili hizo nenda hospitali kwa uchunguzi zaidi.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime